March 7, 2021

 


PEP Guardiola, Kocha Mkuu wa Manchester City amesema kuwa anawahofia mastaa wa Klabu ya Manchester United kutokana na uwezo wao wa kusaka ushindi ndani ya uwanja.

Leo, City itawakaribisha United, Uwanja wa Etihad kwenye mchezo wa Ligi Kuu England ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza walipokutana uwanjani kusaka pointi tatu waligawana pointi mojamoja kwa sare ya bila kufungana jambo ambalo linatoa picha kwamba mchezo wa leo utakuwa ni mgumu kwa timu zote mbili.

United ina rekodi ya kutopoteza mechi 21 ikiwa ugenini huku City wenyeji wakiwa na rekodi ya kushinda jumla ya mechi 21 mfululizo.

Guardiola amesema:"Man United wapo vizuri na wana wachezaji wengi ambao wanaweza kuleta ushindani, kwenye eneo la ushambuliaji Bruno Fernandes ana spidi kama ilivyo kwa  James (Dan) na Rasford," .

Kwa upande wa Ole amesema :"Tunaenda kupambana na timu bora lakini malengo yetu yanabaki ni kushinda kwenye kila mchezo,". 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic