KOCHA mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa amefurahishwa na uwezo mzuri anaouonyesha beki wake wa kati, Peter Muduhwa raia wa Zimbabwe na kutoa sababu zilizomfanya beki huyo kushindwa kupata nafasi ya kucheza ndani ya kikosi hiko tangu asajiliwe.
Muduhwa amesajiliwa na Simba maalum kwa ajili ya michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika mara baada ya kumalizika kwa michuano ya CHAN, ambapo beki huyo alikuwa akikitumikia kikosi cha Timu ya Taifa ya Zimbabwe.
Tangu asajiliwe, Muduhwa hajabahatika kuicheza Simba mechi yoyote ile ya kimataifa ambapo hadi sasa Simba wamecheza mechi mbili dhidi ya AS Vita na Al Ahly.
Akizungumzia nafasi ya beki huyo kocha Gomes amesema kuwa mara kadhaa amekuwa akizungumza naye, ili kumpa hali ya kujiamini zaidi huku akisema kusajiliwa kwa ajili ya michuano ya kimataifa pekee kunamyima nafasi ya kucheza.
“Muduhwa ni mchezaji mzuri sana, anatupa kitu bora sana mazoezini, ni bahati mbaya sana ana leseni ya kucheza ligi ya mabingwa pekee kwani angekuwa na leseni ya kucheza kwenye ligi pia naamini angepata nafasi ya kucheza.
“Huwa naongea naye ili kusaidia kumpa kujiamini zaidi, tayari
kama benchi la ufundi tunaamini sana juu ya uwezo wake na tunaamini ni hazina
kubwa na muhimu ndani ya klabu,” alisema kocha huyo.
Muduhwa amekosa nafasi ya kucheza mbele ya Joash Onyango,
Erasto Nyoni, Pascal Wawa na Kennedy Juma ambao wamekuwa wakicheza mara kwa
mara.
wap lokasa ya mbongo
ReplyDeleteAkaze buti bado nafas anayo
ReplyDeleteDuh! Hata benchi!
ReplyDelete