KLABU ya soka ya Coastal Union kutokea Tanga, leo
imetamatisha mwendo wa michezo 21, bila kufungwa wa vinara wa msimamo wa Ligi
Kuu Bara klabu ya soka ya Yanga baada ya kuibuika na ushindi wa mabao 2-1.
Coastal imeibuka na ushindi huo katika mchezo mkali uliopigwa kwenye dimba la Mkwakwani jijini Tanga.
Kabla ya mchezo wa leo Yanga ilikuwa imecheza michezo 21 ya Ligi Kuu Bara, bila kupoteza mchezo wowote wakishinda michezo 14 na kutoa sare michezo saba.
Licha ya kipigo hicho Yanga bado inasalia katika uongozi wa ligi na pointi zao 49, baada ya kucheza michezo 22.
Hii habari imeandikwa kinyonge sana, usisahau kutuwekea msimamo wa ligi
ReplyDeleteMwandishi mbona Leo kapoa au ndo matatizo ya upumuaji
ReplyDelete😂😂😂
Delete"Nanihino"imevunjwa huko Tanga mpaka nyavu "zikatoboka".Wakubwa wamenielewa.
ReplyDeleteNi bora tumrejeshe Zahera kocha ambae aliisaudia timu kwa hali na mali pamoja na kuzungusha bakuli na ikawa timu yenye kiwango kikubwa na asante yake yake kumtimuwa na kutomlipa haki zake
ReplyDeleteCoastal wamefaidi sana leo, kitu sealed wamefungua wenyewe
ReplyDeleteYanga sasa ni ya kujipigia tu,tundu lishafunguka
ReplyDeleteUkishabakwa lazima ukimbilie Polisi. Au uongo ndugu zangu?
ReplyDelete