March 4, 2021

 


WAKATI akiwa kwenye presha kubwa ya kibarua chake kuota nyasi kutokana na matokeo ambayo hayawafurahishi mabosi wake pamoja na mashabiki wa Yanga, Cedric Kaze amesema hana presha.


Kocha huyo wa Yanga ameweka wazi kuwa aliamua kuifundisha timu hiyo kubwa kwa kuwa anajua kwamba kuna changamoto kwenye kila timu jambo ambalo halimpi mashaka.


Leo Machi 4 ana kazi ya kusaka ushindi mbele ya Coastal Union ambayo kwenye mchezo wa kwanza chini ya Kocha Mkuu, Zlatko Krmpotic ubao ulisoma Yanga 3-0 Coastal Union, Uwanja wa Mkapa.


Kaze amesema:-”Siogopi presha ndani ya Yanga, mimi ni mwalimu na ninatambua kwamba timu kubwa zina presha ndio maana nikakubali kusaini.


“Mashabiki wanahitaji kuona timu inapata matokeo ila haiwezi yote kuwa kwa haraka na pia najua kwamba wanahitaji kuona ninatwaa ubingwa hilo siwezi kuwaambia zaidi ya kuwataka waje uwanjani kushuhudia burudani,” amesema.


Kwenye msimamo wa ligi, Yanga inaongoza ikiwa nafasi ya kwanza na pointi zake ni 49 baada ya kucheza mechi 21.


Inakutana na Coastal Union ya Tanga, Uwanja wa Mkwakwani ikiwa ipo nafasi ya 13 na point zake ni 23.

2 COMMENTS:

  1. Presha unayo tena kubwa tu wala usijidanganye

    ReplyDelete
  2. Subiri leo ufungwe ndio utajua kumbe una presha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic