March 4, 2021



KUELEKEA mchezo wa Jumamosi dhidi ya Al Merrikh ya Sudani, kiungo mshambuliaji wa Simba Luis Miquissone ‘Konde Boy’ juzi jioni, alipewa programu tofauti na wenzake wote ili kumfanya awe fiti kuwavaa Wasudani hao, hii ni baada ya kupata majeraha madogo kwenye mchezo uliopita dhidi ya JKT Tanzania.

Kufuatia majeraha hayo, tofauti na wachezaji wengine Luis aliambiwa azunguke uwanja mara moja, kisha baada ya hapo akapewa mazoezi ya kuendesha baiskeli maalum ya mazoezi, zinazosaidia kuongeza spidi na pumzi ya mchezaji ambalo alifanya kwa dakika 15.

Akizungumzia maendeleo ya mchezaji huyo, kocha mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema: “Kuna baadhi ya wachezaji wetu walipata majeraha madogo kwenye mchezo uliopita dhidi ya JKT Tanzania, miongoni mwao ni Luis.

“Hii ndiyo sababu ya kumpa programu tofauti za mazoezi, kwani ni mchezaji muhimu ndani ya kikosi chetu na ni lazima tuhakikishe anakuwa sawa kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi dhidi ya Al Merrikh, ambao ni wazi tunataka kupata matokeo mazuri,”

Simba tayari imekwishawasili nchini Sudani kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic