March 10, 2021


 IMEBAINIKA kuwa mishahara ya wachezaji wa Klabu ya Real Madrid kwa wachezaji walioshindwa kukidhi matarajio ya mashabiki, Gareth Bale na Eden Hazard ndiyo wanakomba kitita kikubwa zaidi klabuni hapo.

 

 Real Madrid ni timu ya soka ya pili duniani kwa kulipa mishahara mikubwa, ikiwa nyuma ya Barcelona pekee. 


Bale anaongoza akiwazidi wenzake mbali sana akipokea kitita cha pauni 650,000 (Sh bilioni 2) kila wiki, licha ya kuwa hayupo katika mipango ya kocha Zinedine Zidane na ameshapelekwa kwa mkopo Tottenham.

 

 Tottenham ilikubali kuchangia nusu ya mshahara wa Bale ili kumnasa kwa mkopo, ikimaanisha kuwa inatoa paun 325,000 kila wiki huku Madrid nao wakitoa kiasi kama hicho.

 


Eden Hazard, anafuatia akiwa anachukua mshahara wa pauni 416,000 (Sh bil 1.3) kwa wiki. Mbelgiji huyo, mwenye miaka 30, amecheza mechi 24 tu za La Liga tangu ajiunge akitokea Chelsea mwaka 2019 kwa donge nono la pauni milioni 88 ambalo linaweza kufikia hadi pauni mil 150.

 

 Gwiji wa klabu hiyo, beki Sergio Ramos anachukua mshahara wa pauni 312,000 kwa wiki, wakati viungo Toni Kroos na Luka Modric wakipokea pauni 210,000 kila mmoja.

 

 Wachezaji wengine 12 wa klabu hiyo wanapokea kitita cha pauni 100,000 au zaidi kila mmoja. Straika aliyefeli Luka Jovic ambaye sasa anacheza kwa mkopo Eintracht Frankfurt, anapokea pauni 175,000 kwa wiki huku Karim Benzema akipokea pauni 166,000.

 


Thibaut Courtois, Raphael Varane na Marcelo wanapokea pauni 150,000 kwa wiki kila mmoja. Dani Carvajal, Isco, Alvaro Odriozola, Lucas Vazquez, Marco Asensio, Eder Militao na Borja Mayoral ni wachezaji wengine wanaopokea kitita cha pauni 100,000 au zaidi kwa wiki.

 


Wanaopokea chini ya hapo ni Andriy Lunin (pauni 50,000), Ferland Mendy (pauni 53,000), Federico Valverde (pauni 62,000).


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic