March 10, 2021


 IKIWA leo wanatarajia kukutana Uwanja wa Mkapa kuna vita kubwa ya ufungaji kwa wachezaji wa timu mbili Simba inayonolewa na Didier Gomes pamoja na Tanzania Prisons inayonolewa na Salum Mayanga.

Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, Simba wapo nafasi ya pili wakikusanya pointi 45 baada ya kucheza mechi 19, huku Tanzania Prisons ikiwa nafasi ya 10 na pointi 27.

 Wakati Simba na Prisons wakienda kupambana, takwimu zinaonyesha kwamba, washambuliaji wawili wa Simba, John Bocco na Chris Mugalu, idadi yao ya mabao ni sawa na ile iliyofungwa na timu nzima ya Prisons katika ligi kuu msimu huu.

 

Bocco mwenye mabao tisa na Mugalu matano, jumla yake ni 14 ambayo ndiyo yamefungwa na timu nzima ya Prisons msimu huu huku kinara wao akiwa Jumanne Elfadhili mwenye matatu.


Simba jumla imefunga mabao 45 na inaongoza kwa timu yenye safu kali ya ushambuliaji kwa msimu wa 2020/21 kwa kuwa hakuna zile zote ambazo zipo ndani ya tano bora hazijafikia idadi hiyo.


Yanga inayoongoza ligi safu yake ya ushambuliaji imefunga jumla mabao 36 na Azam FC ambayo ipo nafasi ya tatu imefunga jumla ya mabao 31.


Hivyo leo ukiweka kando vita ya pira gwaride na pira biriani kuna vita ya kusaka rekodi kwa upande wa wacheka nyavu kiujumla ndani ya dakika 90.


Ikumbukwe kwamba kwenye ule mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela, Prisons iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic