March 10, 2021


 MSHINDO Msolla, Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga amesema kuwa wale ambao wanasema kwamba mdhamini wao Kampuni ya GSM hana msaada ndani ya timu hiyo huyo atakuwa sio mwenzao kwa kuwa haoni kile ambacho kinafanywa na mdhamini huyo.

Hivi karibuni baadhi ya mashabiki wamekuwa wakitajwa kulaumu uwepo wa wadhamini wa GSM wakidai kwamba hao wamekuwa watendaji badala ya uongozi jambo linalofanya timu kuyumba.

Msolla ameweka wazi kwamba ndani ya Yanga kila mmoja anatimiza wajibu wake kwa kufanya kile ambacho kinamhusu bila ya kuingiliana katika madaraka.

"Kila mmoja anafanya kazi yake, ikiwa kuna shabiki ambaye hataki GSM kuwa ndani ya Yanga huyo atakuwa sio mwenzetu kwa sababu hatambui yale ambayo wadhamini wetu wanafanya.

"Kwetu sisi sio wadhamini pekee bali wamekuwa ni patna katika kazi zetu na kila mmoja anatimiza majukumu yake kwa wakati.

"Mazingira ambayo tulianza nayo awali yanajulikana ila kupitia hawa GSM wameweza kulipa kambi ambayo timu imekuwa ikiweka, tulianza nao pale Legency alilipa miezi sita na kwa sasa tupo Avic ni mwaka mzima amelipa," amesema.

Chini ya Injinia Hersi Said ambaye ni Mkurugenzi wa Uwekezaji Kampuni ya GSM, Yanga imeweza kuhama kambi kutoka Legency na sasa ipo Kigamboni ambapo inaendelea na maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara.

13 COMMENTS:

  1. Viongozi mmebakia kama vikaragosi hamna uwezo wa kuamua chochote.GSM ndio wamekuwa waamuzi. Nugaz ni mwajiriwa wa nani?GSM au Yanga.Kila akizungumza anazungumzia brand ya GSM kama kwamba GSM ni klabu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani kule kwa nanii mbwa gani anakohoa zaidi yake nanii tu? Viongozi wa nanii wamekuwa wafukuza upepo tu hawana cha kuongea zaidi ya nanii tu.halafu unapost makeup hapa.

      Delete
    2. Wewe choko kweli Mo haingilii utendaji Simba Wala masuala ya usajili kwani pale Chelsea mwenye sauti Nani Kama sio Abramovich ulishamuona anaingilia masuala ya usajili yeye anachofanya anatoa fedha baada ya kujiridhisha kutoka kwa management ndivyo anavyofsnya Mo,Sasa GSM utendaji wao, usajili wao alafu unataka kumfananisha na Simba hopeless kabisa

      Delete
    3. Huyo utopolo kashadata na kuolewa kabisa GSM, hajui kutofautisha MO na GSM

      Delete
    4. Hivi pale Simba viongozi wa kuchaguliwa wana nguvu gani? Hata kujulikana hawajulikani. Bodi nzima ni wafuasi wa Mo! Ofisi ya Simba imehamia kwenye ofisi za Mo Enterprises, pale Msimbazi pamebaki gofu, jengo limebaki kuwa makazi ya popo, bundi, nge, sisimizi na nyoka. Kweli nimeamini. NYANI HAONI KUNDULE!!

      Delete
  2. KUTOKA LEGENCY MPAKA AVIC, SAA HZI TIMU INAONGOZA MECHI PUMBA KABISA. KUTOKA MWAMBUSI KAJA NIZA, RIEDO BIDDEN KAJA EDEM MOROTSI.....SAA HIZI KAJA MEXIME NA MWAMBUSI TENA. MNAFUKUZA METACHA,

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umeandika nini?Hebu kaa chini uandike vizuri tukuelewe maana ulichoandika unakielewa mwenyewe

      Delete
    2. Hatushangai utopolo wanaona maluelue tu moja nambili hazikai

      Delete
  3. Anayemlipa mpiga zumari ndio anayechagua nyimbo GSM ndio anayefanya maamuzi Viongozi wa Yanga ni vikaragosi tu.Jiulize Nugaz huwa anasema nini ?Ni lazima alinde chapa ya GSM-brand.Kama ni wadhamini tu basi kwanini asiseme Sports Pesa au Taifa Gas.GSM ndio wanaoamua kila kitu.

    ReplyDelete
  4. Kwa kweli bila GSM Yanga ingekuwa timu ya daraja la kwanza.Msaada anaoutoa GSM kwa Yanga kila mshabiki anauona na walitakiwa kuupongeza.

    ReplyDelete
  5. Acha gsm wafanye kazi yao mtakaa vibarazani kutwa kuumiza kichwa,, Simba na na yanga zishaingia kwenye mitego cha msingi ni kuangalia timu ifanye vizuri furaha iendelee....mmekunywa chai lakini

    ReplyDelete
  6. Ukweli Mwambusi sio kocha mzuri.Kajitoa eti Afya afu anarudi.Kama viongoz Wanaakili nzuri huyo ndio shida.Aje kocha yoyote ila kama uyo yupo bado tuu ni shida.Mfuatilieni vzr.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic