March 10, 2021


 KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kimeanza maandalizi kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, (AFCON) chini ya Kocha Mkuu, Kim Poulsen. 

Kambi ilianza Machi 8 na jana Machi 9 walifanya mazoezi kwa mara ya kwanza Uwanja wa Mkapa ambapo moja ya mchezaji ambaye alikuwa kwenye mazoezi hayo ni mkongwe Kelvin Yondani.

Kikosi chenye jumla ya wachezaji 40 kilitangazwa na Poulsen, Februari 26 ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi hayo ambayo tayari yameshaanza.

Kocha huyo amesema kwamba anaamini watafanya vizuri kwenye mechi zao pamoja na kufanya maandalizi kwa wakati.

"Wachezaji tutakuwa nao na kila mmoja atafanya kazi kwa kutimiza majukumu yake uwanjani, kila kitu kitakuwa sawa hivyo mashabiki watupe sapoti," . 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic