March 10, 2021


 PATRICK Aussems maarufu kwa jina la uchebe ambaye aliweza kuifundisha timu ya Simba kwa mafanikio makubwa anatajwa kuingia kwenye rada za Yanga.

Kwa sasa kikosi cha Yanga ambacho kinaongoza Ligi Kuu Bara kikiwa na pointi 50 baada ya kucheza jumla ya mechi 23 kipo chini ya Juma Mwambusi.

Cedric Kaze aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo baada ya kuongoza kwenye mechi 18 za ligi akishinda 10, sare 7 na kupoteza moja amechimbishwa kikosii hapo Machi 7 kutokana na kile ambacho kimeelezwa kuwa mwendo mbovu wa timu hiyo.

Aussems kwa sasa yupo nchini Kenya anakinoa kikosi cha AFC Leopards hivyo ikiwa Yanga watakuwa kwenye hesabu za kumpata itawalazimu kuvunja mkataba wake ndani ya kikosi hicho.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Mshindo Msolla amesema kuwa kwa sasa wameanza mchakato wa kumtafuta mrithi wa Kaze na wanaamini kwamba watampata hivi karibuni.

3 COMMENTS:

  1. AFC LEOPARDS AMEKATAA, TAARIFA KUTOKA GOAL.COM ZA UHAKIKA KABISA ZIMESEMA HILO

    ReplyDelete
  2. Mchukuweni na Mungu akipenda atakupatieni makubwa lakini kwa muda huu mdogo iliyobakia msitaraji makubwa, hivo msifanye haraka ya kumtimuwa pale mambo hayatokuwa mnavoyararajia

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic