MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa muda wa kujifunza kwa nyota wake Nicolas Pepe umeisha hivyo anapaswa afanye kazi kweli.
Pepe alitua Arsenal kwa kuweka rekodi ya usajili wake kwa dau la pauni milioni 72 akitokea Klabu ya Lille ila mambo yake yamekuwa tofauti uwanjani.
Hivi karibuni aliisaidia kuifungia timu yake mabao dhidi ya Salvia Prague na kutinga hatua Nusu Fainali ya Europa League.
Arteta amekiri kuwa winga huyo muda wa kujifunza mambo umekwisha kwa sasa anatakiwa kupambana.
"Nico ana uwezo lakini uwezo wake wake unategemeana na yeye mwenyewe. Tunaweza kumsaidia tunavyotaka ila anatakiwa kuweka akili yake sawa na kujua anatakiwa kupambana," .
0 COMMENTS:
Post a Comment