April 18, 2021


 JUMA Mwambusi, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wachezaji wake waliweza kushinda na kucheza vizuri kwa sababu walifuata maelekezo ambayo walipewa.

Jana Aprili 17, Yanga ilimalizana na Biashara United Uwanja wa Mkapa kwa ushindi wa bao 1-0 na kusepa na pointi tatu.

Ni Yacouba Sogne alipachika bao la ushindi kipindi cha pili baada ya dakika 45 kukamilika kwa miamba hiyo yote miwili kushindwa kufumania nyavu za wapinzani wao.

Ushindi huo unaifanya Yanga kuzidi kujikita kileleni ikiwa na pointi 54 baada ya kucheza mechi 25 inafuatiwa na Azam FC iliyo nafasi ya pili na pointi zake ni 50 baada ya kucheza mechi 26.

Biashara United ipo nafasi ya nne na imebaki na pointi zake 40 huku watani wa jadi wa Yanga Simba ngome yao ni nafasi ya tatu na pointi zao ni 49 baada ya kucheza mechi 21.

Mwambusi amesema:"Wachezaji wameweza kufuata maelekezo ambayo nimewapa na wamefanya vizuri jambo ambalo ni furaha kwangu na kwao pia.

"Kikubwa ninawapa pongezi kwa sababu haukuwa mchezo mwepesi ulikuwa na ushindani mkubwa," .

1 COMMENTS:

  1. Sababu ya kushindwa kwa kuwa mnae kocha anaestahaki kuendelea na timu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic