April 24, 2021


GEORGE Lwandamina, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Mchezo huo wa mzunguko wa pili unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 2:15 usiku ambapo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika zote 90 kutokana na timu hizo kuwania ubingwa.

Azam FC ipo nafasi ya tatu na ina pointi 51 baada ya kucheza jumla ya mechi 27 inakutana na Yanga ambayo ipo nafasi ya kwanza na pointi 57 baada ya kucheza jumla ya mechi 26.

Lwandamina ambaye amewahi kuifundisha Yanga amesema kuwa wanaamini kwamba wataingia kwa mfumo tofauti katika kutafuta matokeo chanya kwenye mchezo huo.

"Wachezaji wapo tayari na tunatambua kwamba utakuwa ni mchezo wenye ushindani hivyo utapambana ili kupata pointi tatu hatuna mashaka tunaamini tutapata matokeo chanya," amesema.

Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Azam Complex ubao ulisoma Azam 0-1 Yanga na bao lilifungwa na Deus Kaseke.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic