April 24, 2021


 NYOTA wanne ndani ya Yanga wanahesabu siku tu kabla ya kufungashiwa virago ili kuweza kusepa kikosini hapo baada ya kushindwa kuonyesha kile ambacho kilitarajiwa.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi ambaye alirithi mikoba ya Cedric Kaze kwa sasa inajiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, kesho majira ya saa 2:15.

Habari kutoka ndani ya Yanga zimeeleza kuwa mpango mkubwa uliopo kwa sasa ndani ya kikosi hicho ni kufanya maboresho mapya kwa kuwaondoa wachezaji ambao hawana mchango mkubwa.

"Kweli kwa sasa Yanga ipo kwenye hesabu za kufanya maboresho ya kikosi hicho ambapo tayari wapo wachezaji ambao wameambiwa kwamba hawataongezewa mikataba hivyo wanasubiri siku za kuondoka.

"Fiston Abdulazack huyu mkataba wake unaisha kuongezewa mkataba wake ni ngumu, Michael Sarpong asibopadilika kwenye mzunguko huu wa pili basi safari inamuhusu.

"Farid Mussa amekuwa kwenye kiwango cha kawaida tofauti na ilivyotarajiwa, Wazir Junior naye hana maisha marefu na anaweza kutolewa kwa mkopo, hivyo msimu ujao hawa jamaa wanaweza kuwa na maisha sehemu nyingine" ilieleza taarifa hiyo.


6 COMMENTS:

  1. Acha kutunga story ili kuwachanganya akili wachezaji wa Yanga watoke mchezoni, huo ni uongo mkubwa ligi haijaisha na msimu haujaisha mchezaji bado anahitajika kumalizia msimu halafu unamwambia eti ataachwa!! Unadhani akili yake itakuwa na utulivu!!! Wewe doctor akikuambia utakufa baada ya wiki hii kuisha, utakuwa na utulivu?? Tumia busara kuandika stori zako usiandike ili kuwanufaisha Simba ili tarehe 8 wacheze na wachezaji wa Yanga wasiojiamini. Kama Simba wanakulipa kuandika propaganda za kuwavuruga wachezaji wa Yanga jua umefeli na huo ujanja ni wakizamani sana.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyu..Ni...SALEH JEMBE...kazi kupiga majembe Tu..! Kila apatalo sokoni yeye hutuma Tu bila ya kuhakiki..!

      Delete
  2. Hivi viandishi ni vipumbavu Sana mpaka vinakera ,Usimba umewajaaas

    ReplyDelete
  3. Huo uandishi sio ndio maanahayati rais magufuri alikua hapendi waandishi wa habari wajinga Kama hawa wanaojua kuropoka tu ninachoomba uwe na staa kidogo unavyoongea hivo ili tupoteze mchezo acha Mambo yako na Nina uhakika unetumwa na Simba na tarehe nane kipigo kipo pale pale

    ReplyDelete
  4. Huwo ni uzushi tu waandishi wengine hawana akili wanawaza kila kitu ni chakuandika upuuzi tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic