April 18, 2021


BEKI tegemezi wa pembeni ndani ya kikosi cha Mtibwa Sugar, Hassan Kessy amesema kuwa yupo tayari kusaini kwenye timu yoyote ambayo itahitaji saini yake hata wakiwa ni mabosi wake wa zamani, Yanga.

Nyota huyo alirejea Mtibwa Sugar msimu huu akitokea Klabu ya Nkana FC ya Zambia ambayo alijiunga nayo akitokea Klabu ya Yanga.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kessy amesema kuwa kazi ya mchezaji ni mpira hivyo hana tatizo ikiwa atapata ofa kutoka timu nyingine.

“Mimi ni mchezaji na nipo tayari kucheza popote kikubwa ni maslahi pamoja na makubaliano hivyo hata ikiwa ni Yanga sina tatizo nao mimi nitacheza.

“Kwa sasa nipo hapa Mtibwa Sugar na tunazidi kupambana ili kupata matokeo chanya kwani kila mechi inakuja tofauti na tunaamini kwamba tutapata matokeo kwenye mechi zetu zijazo,” amesema Kessy.

Nyota huyo alikuwa anatajwa kujiunga na Yanga kabla ya kuibukia Mtibwa Sugar akitokea Zambia ila mambo yalibadilika akaibuka Mtibwa Sugar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic