April 25, 2021

 


TANGU ajiunge na timu ya Simba, Septemba 15, 2019, Clatous 
Chama raia wa Zambia amecheza jumla ya michezo 112, na kuwa na mchango mkubwa katika kikosi hicho.

Kiungo huyo mchezeshaji amekuwa na umuhimu mkubwa katika kikosi cha Simba kuanzia katika michuano ya ndani ya Tanzania na ile ya Kimataifa, akiwa msaada katika kubeba mataji ya Ligi Kuu Bara na Kombe la FA.

Ana jumla ya pasi za mwisho 45 tangu ajiunge na kikosi cha Simba hiyo ni kwenye mashindano yote akitokea Power Dynamos ya Zambia.

Kwa msimu huu mpaka sasa katika Ligi Kuu Bara, Chama ameshafikisha jumla ya asisti 11 na bado zimesalia mechi za kuendelea kuchezwa kwa Simba na ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Didier Gomes.

Katika mabao Chama amefunga jumla ya mabao 30 kwenye michezo yote ikiwemo ile ya Ligi ya Mabingwa ambayo kwa msimu huu Simba imeingia hatua ya robo fainali.



4 COMMENTS:

  1. Ndo maana mpo kimya siku hzi hamseni tena carlinho amfunika chama

    ReplyDelete
  2. Chama is Simba's back bone for his club's successes, who so far can be compared with none, not only in Tanzania, but probably in the entire of East Africa. We wish him the best as he surges ahead with his professions

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mtoa comment alikuwa sahihi Clatous Chama alijiunga na Simba 2018 muda mfupi kabla Dimba hawaenda Uturuki kwenye pre-season camp na siyo Sept 2019. Msiifute comment sahihi

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic