April 20, 2021


 IMEELEZWA kuwa nyota wa Yanga, Fiston Abdulazak ameitelekeza familia yake katika masuala ya matunzo jambo ambalo limemfanya mke wake pamoja na watoto wawili kutua Dar kudai haki zao.

Habari kutoka kwa mtu wa karibu wa na staa huyo mwenye mabao mawili ndani ya Yanga zimeeleza kuwa mke wake pamoja na watoto hao wapo Bongo kwa ajili ya kuhitaji kupata malezi.

Mtoa taarifa huyo amesema kuwa Mwanamke huyo yupo Tanzania kwa muda wa siku kadhaa na ameambatana na mwanasheria wake ili kumchuka staa huyo kwenda naye mahakama ya Burundi.

"Mke wa Fiston yupo Dar hapa kwa muda sasa na amekuja na watoto wawili na Mwanasheria wake kuja kudai haki zake baada ya kudai Fiston aliwaacha bila msaada wowote wala kutuma fedha kwa ajili ya matumizi ya watoto wake," ilieleza taarifa hiyo.

Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla alipotafutwa alisema kuwa :"Mimi siwezi kuzungumzia chochote kwenye suala hilo," .

Alipotafutwa Fiston hakuweza kujibu ujumbe aliotumiwa.

Chanzo:Championi

2 COMMENTS:

  1. Ni masuala ya kifamilia ila yatampotezea umakini ktk kazi yake, bora alitatue

    ReplyDelete
  2. Kwani hapati mshahara au?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic