KOCHA Mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kuwa hana tatizo na mshambuliaji wake namba moja, Sergio Aguero ikiwa atajiunga na timu inayoshiriki Premier League.
Aguero anasepa ndani ya City msimu utakapoisha kwa kuwa mkataba wake utakuwa umekamilika na tayari mabosi zake na mchezaji wamekubaliana kwamba hawatamuongezea mkataba mpya mshambuliaji huyo ambaye amedumu katika timu hiyo kwa miaka 10.
Nyota huyo ambaye ni mfungaji bora wa muda wote ndani ya City akiwa amefunga jumla ya mabao 257 amekuwa akihusishwa kujiunga na Klabu ya Chelsea pamoja na Manchester United ambazo zinampigia hesabu staa huyo mwenye miaka 32, raia wa Argentina.
Pia baada ya City kutangaza kwamba hawatamuongezea mkataba Arguero mauzo ya jezi za Arguero yameongezeka kwa kiasi kikubwa kutokana na mashabiki kuthamini mchango wa staa huyo ambaye anatarajiwa kunyanyua taji lake la tano msimu huu kwa kuwa ametwaa mataji manne ya Ligi Kuu England.
"Sisi wote tunamtakia kila la kheri yeye, tutaheshimu maamuzi ambayo ataamua tunajua kwamba itakuwa ni bora kwake na familia pia, tuna kazi ya kumtafuta Arguero mwingine tena ila kile ambacho atakiamua yeye sisi hatuna tatizo naye, kizuri kwake ni kizuri kwetu pia.
"Sergio ni mchezaji mwenye upendo na anampenda kila mtu, ana vitu vyake vya kipekee na mbali na ubora pamoja na kipaji ambacho anacho, ninamjua yeye na ninaelewa kwamba anahitaji kuwa bora katika kile ambacho anakwenda kukifanya," .
0 COMMENTS:
Post a Comment