April 10, 2021


 KAIMU Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Juma Mwambusi amesema kuwa wataingia kwenye mchezo wao dhidi ya KMC kwa kushambulia na kujilinda kwa tahadhari ili kuibuka na ushindi katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Leo majira ya saa 1:00 usiku, Yanga ambao ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 50 baada ya kucheza mechi 23 wanatarajiwa kumenyana na KMC iliyo nafasi ya tano ikiwa na pointi 35 katika mchezo wa pili ambao ni wa mzunguko wa pili.

Mchezo ule wa kwanza msimu huu wa 2020/21 walipokutana katika mzunguko wa kwanza, Uwanja wa CCM Kirumba ubao ulisoma KMC 1-2 Yanga.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mwambusi amesema kuwa wanatambua kwamba KMC ni timu imara hasa inapokutana na Yanga ila wapo tayari kwa ajili ya mchezo.

"Tunajua kwamba KMC ni timu imara inapokutana na Yanga ila tutapambana kwa ajili ya kupata matokeo. Tutacheza kwa kushambulia ili kupata ushindi hatutapaki basi ila tutajilinda kwa tahadhari.

"Niliona mchezo uliopita ambao tuliwafunga hivyo kwa maandalizi ambayo tumeyafanya nina amini kwamba wachezaji wana kazi ya kuonyesha kile ambacho tumekifanyia kazi katika mazoezi," amesema.

Kwa upande wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kila kitu kipo sawa hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu yao.

1 COMMENTS:

  1. Mwambusi acha uongo. KMC ni ving'ang'anizi kwa kila timu wanayo kutana nayo na hasa SIMBA na wala sio Utopolo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic