April 23, 2021


 BADRU Mohammed, Kocha Mkuu wa Gwambina FC amesema kuwa anatambua kesho ana mchezo mgumu dhidi ya Simba ila hana mashaka kwa kuwa lazima akutane nao na dakika 90 zitaongea.

Gwambina inakutana na Simba ambayo imetoka kushinda mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba huku wao wakitoka kupoteza kwa kufungwa mabao 3-1 dhidi ya Yanga, Uwanja wa Mkapa.

Mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa na Simba, ubao ulisoma Simba 3-0 Gwambina na kuwafanya Simba kusepa na pointi tatu ilikuwa ni zama za Sven Vandenbroeck ambaye alisepa  na timu  ya Simba ipo chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes kwa sasa.

Badru amesema:"Gwambina ni timu hodari na inacheza mpira vizuri, nina amini kwa ambaye anajua mpira ameona namna ambavyo iliweza kucheza mbele ya Yanga hata tulipocheza na KMC kuna mambo ambayo niliyaona.

"Tunawaheshimu Simba ila inabidi wajue kwamba wanakuja nyumbani, hapa hatuna mashaka tutapambana kupata matokeo, dakika 90 zitaongea.

"Kuhusu ratiba kwangu ninaona kwamba hii ni kawaida na imepangwa na timu zote lazima tucheza nazo, hakuna mashaka," amesema.

Gwambina FC kwenye msimamo ipo nafasi ya 12 ina pointi 30 inakutana na Simba iliyo nafasi ya pili na pointi 55 hivyo ni vita ya timu inayosaka ubingwa wa ligi pamoja na ile inayopambana kujinasua kwenye nafasi ya kushuka daraja.

1 COMMENTS:

  1. Mdomo utakuponza we kocha, waulize wenzako..... kumbuka Unacheza na Simba sio utopolo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic