April 24, 2021

 


BAADA ya mabosi wa Yanga kumtambulisha rasmi mrithi wa mikoba ya Cedric Kaze kwa mashabiki wao tayari ameanza kazi kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho kuelekea kwenye mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.

Nasreddine Nabi ambaye ni raia wa Tunissia amepewa dili la mwaka mmoja na nusu kukinoa kikosi hicho ambacho kilikuwa mikononi mwa Juma Mwambusi aliyekuwa akikaimu nafasi ya Kaze iliyoachwa wazi tangu Machi 7, 2021.

Raia huyo wa Tunissia jana alianza kuwanoa nyota wa kikosi hicho wakiongozwa na kipa Faroukh Shikhalo, Ditram Nchimbi, Kibwana Shomari, Feisal Salum, Saido Ntibanzokiza kwa ajili ya mechi ya kesho ya ligi dhidi ya Azam FC.

Yanga ikiwa inaongoza ligi baada ya kucheza mechi 26 kesho Uwanja wa Mkapa inakazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Azam FC kwenye mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Azam ipo nafasi ya tatu na pointi 51 inakutana na vinara wenye pointi 57 jambo ambalo litaongeza ushindani.

Kwenye mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Azam Complex, ubao ulisoma Azam 0-1 Yanga.

Nabi amesema kuwa anatambua wachezaji wake wapo imara na amewaambia kwamba wana kazi ya kuonyesha vitendo kwenye mechi zote.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic