MOHAMED Badru, Kocha Mkuu wa Gwambina FC amesema kuwa hawana hofu na mchezo wao wa ligi dhidi ya KMC wanaamini watapata ushindi.
Gwambina imetoka kushinda mabao 4-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga uliochezwa Uwanja wa Gwambina Complex inakutana na KMC ambayo imetoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Yanga.
Kwenye msimamo wa ligi, Gwambina ipo nafasi ya 9 na pointi zake ni 30 wakati wenyeji wao KMC wapo nafasi ya 6 na pointi 36.
Badru amesema:"Hakuna unyonge kwa sasa kwenye timu yangu, naona wachezaji wanajiamini na wanahitaji pointi tatu kwenye mchezo wetu dhidi ya KMC.
"Tunawaheshimu wapinzani wetu kwa kuwa ni timu imara ila haitufanyi tuwe na mashaka baada ya dakika 90 tutajua nini ambacho tumekivuna," amesema.
Mchezo huo utachezwa Ijumaa, Aprili 16, Uwanja wa Uhuru.
0 COMMENTS:
Post a Comment