April 14, 2021


 JUMA Mwambusi, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa sababu kubwa iliyomfanya amtoe  Tonombe Mukoko na nafasi yake kuchukuliwa na mshambuliaji Ditram Nchimbi ilikuwa ni kuongeza nguvu ya mashambulizi kwa wapinzani wao.

Aprili 10 wakati Yanga wakigawana pointi mojamoja na KMC kwenye mchezo wa ligi baada ya ubao kusoma, Yanga 1-1 KMC Nchimbi alitumia dakika 14 kuonyesha makeke yake. 

Ilikuwa dakika ya 76 ambapo aliingia kuchukua mikoba ya kiungo mshambuliaji Tonombe Mukoko, jambo hilo limekuwa likilalamikiwa na baadhi ya mashabiki ambao wamekuwa wakisema kwamba hawaelewi ilikuaje Nchimbi akaingia.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mwambusi amesema kuwa sababu kubwa za kufanya mabadiliko ni za kiufundi na ziliweza kuleta matokeo.

"Niligundua kwamba tumekuwa hatupeleki mashambulizi kwa wapinzani wetu kwa kasi na haraka na kwa kuwa tulikuwa tunahitaji ushindi ilikuwa ni lazima tushambulie.

"Wale ambao waliingia wote walikuwa kwenye mpango ndio maana unaona kwamba baada ya hao kuingia ikiwa ni pamoja na Nchimbi kuna mabadiliko ambayo yalikuwa yanaonekana.

"Ushindani kwenye ligi ni mkubwa na awali niliweka wazi kwamba tunapokutana na KMC wapinzani wetu wamekuwa ni bora, lakini nasi pia bado tuna kazi ya kufanya kwa ajili ya mechi zijazo," amesema.

Yanga kwa sasa inajiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Biashara United ambao unatarajiwa kuchezwa Aprili 17, Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku.

4 COMMENTS:

  1. Mabadiliko hayakuwa ya kiufundi huwezi mtoa kiungo na kumweka mshambuliaj ina maana hapo unaenda kupunguza muunganiko wa timu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic