UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa kwa sasa nafasi ambayo wanafikiria ni ile ya kwanza iliyo mikononi mwa Simba kwa kuwa hawana presha na ile ya pili iliyo mikononi mwa Yanga.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa tayari
kikosi kimerejea kwenye ubora wake na wanaamini kwamba bado wana nafasi ya
kutwaa ubingwa kutokana na mechi ambazo wanazo.
Aprili 25, Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina ililipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 na Yanga kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex na mpleleka maumivu alikuwa ni Deus Kaseke.
Azam nao walishinda bao 1-0 mbele ya Yanga na mpeleka maumivu alikuwa ni Prince Dube ambaye ni kinara wa utupiaji akiwa na mabao 12.
Zaka amesema:-“Nafasi
ambayo tunaifikiria ni ile ya kwanza, hatuna haja ya kuangalia yule ambaye yupo
chini ya hapo, mawazo yetu ni ya mbali na tunaamini kwamba tutafanya vizuri
hilo lipo wazi kwani wachezaji wamekuwa kwenye ubora.
“Washindani
wetu wajipange kwani kila mechi kwetu itakuwa fainali na ushindani ni mkubwa
hilo lipo wazi hivyo bado tunaamini kwamba tutafanya vizuri na kuweza kutimiza
jambo letu,” amesema Thabit.
Kwenye msimamo Azam FC ipo nafasi ya tatu na pointi zake ni 54, Yanga namba mbili na pointi 57 wakati vinara ni Simba wenye pointi 61.
0 COMMENTS:
Post a Comment