April 27, 2021


 WAKATI ikielezwa kuwa kinara wa utupiaji ndani ya Ligi Kuu Bara kwa sasa Prince Dube anapigiwa hesabu na timu mbalimbali ndani ya Bongo na nje ya nchi nyota huyo ameweka wazi kwamba hafikirii kwenda popote.

Miongoni mwa timu ambazo zilikuwa zinatajwa kuhitaji saini ya nyota huyo raia wa Zimbabwe mwenye mabao 12 na pasi tano za mabao ni pamoja na Yanga, Simba kwa nje ya Bongo Raja Casablanca ilikuwa inatajwa kuhitaji saini yake.

Nyota huyo mpole ukimuona ila katili akiwa karibu na nyavu hata nje ya 18, ameweka wazi kwamba anafurahia maisha yake ndani ya Azam FC kwa kuwa wanampa kitu cha utofauti.

"Furaha yangu ni kuwa ndani ya Azam FC, sifikirii kwenda sehemu nyingine tofauti na hapa hivyo ninaweza kusema kwamba ninafurahi kuwa Azam FC.

"Sapoti na nafasi ambayo ninaipata Azam FC ni kubwa hivyo nitazidi kupambana kwa ajili ya timu yangu," amesema Dube.

Aprili 25,2021 aliwafunga wapinzani wao Yanga ikiwa ni bao lake la kwanza msimu wake wa kwanza ndani ya ligi. Mchezo wake wa kwanza ndani ya mzunguko wa kwanza walipokutana na Yanga walipoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Katika mchezo huo Dube aliumia mkono na alikaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita akitibu mkono wake.

1 COMMENTS:

  1. Ikiwa watani mwaka jana ilishindwa bei ya Sure Boy vipi leo iweze bei ya Prince ambaye huyo vilevile die wa kubeza na kutimuliwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic