April 27, 2021

 


HERRY Mzozo ambaye ni meneja wa beki wa kushoto wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, amesema kuwa mchezaji huyo anawindwa vikali na klabu za kutoka nchini Afrika Kusini ‘Sauz’. 

Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, beki huyo amefanikiwa kucheza michezo yote akianza kikosi cha kwanza.

Pia hata wakati Simba ikitwaa taji la kwanza la SimbaSuper Cup likiwa ni taji la kwanza kwa Kocha Mkuu, Didier Gomes aliweza kupata nafasi ya kucheza mechi hizo na kuonyesha kiwango kizuri.

 

Iliripotiwa kuwa, anatakiwa na Yanga ambayo inahitaji kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho.


Mzozo alisema kuwa nyota huyo mkataba wake unakaribia kuisha na bado hajaongeza mkataba mwingine.

 

“Tshabalala bado hajasaini mkataba na Simba, mkataba wake wa awali umesalia miezi miwili ili umalizike na kuna ofa kutoka katika timu za Afrika Kusini ambazo zimeonyesha nia kuwa zinamuhitaji.


 "Kuhusu Yanga bado sijapata ofa rasmi, nasikia tu tetesi kuwa wanamhitaji.Lakini Simba bado wana nafasi kubwa ya kumuongezea mkataba kwa kuwa bado ni mali yao ila kama hizo timu kutoka Afrika Kusini zitafika makubaliano mazuri basi sisi hatutakuwa na shida, tutafanya biashara,” alisema meneja huyo.


Hivi karibuni kuhusu sakata hilo, Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Simba, Barbara Gonzalez, alisema:

 

“Tunajua wazi kuwa beki na nahodha wetu Tshabalala mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu na tayari zipo timu ambazo zinavutiwa kumsajili lakini niweke wazi kuwa huyo bado ni mchezaji wetu kwa kuwa ana mkataba na Simba, lakini uongozi una matarajio makubwa ya kumpa mkataba mpya ili aendelee kuitumikia klabu yetu.

3 COMMENTS:

  1. Eee Yanga ikiwa ni kweli, mns ubavu gani wa kumchomoa mchezaji yeyote wa Mnyama. Mliweza wakati ule tu alipokuja Mnyama taaban kipesa na si sasa na katika kuanzia miaka hii ni Mnyama tu ndie alieweza kumchomoa kwengineko aliowataka

    ReplyDelete
  2. Huyu wakala anapenda kelele sana, nadhani hajui kazi yake

    ReplyDelete
  3. kunanyakati inabidi mameneja wa badilike kipindi mchezaji yupo kwenye kiwango ndo unaanza kuwa msemaji badala ya kuwa msimamizi katika kuendeleza kipaji chake leo hii tunaliona kwa herry mzozo tukirudi nyuma kuna wachezaji walipita simba nakuonyesha viwango bora na waliaza kuringa kuongeza mkataba mpya wakisema wanaenda kutafuta changamoto sehemu nyingine mfano ni Banda yupo A.S hivi leo kuna mtu anataarifa zake au ndo vile yupo nje tukirudi kwa Kessy naye leo yupo mtibwa anapambana huko

    NB mameneja waache kujiona mungu watu kipindi mchezaji wake yupo bora

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic