April 28, 2021

INAELEZWA kuwa Mohamed Hussein,'Tshabalala' mkataba wake upo karibuni kuisha na hakuna mazungumzo ambayo yameanza na mabosi wake hao ambao ni mabinhwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mtoa taarifa ameeleza kuwa Tshabalala ambaye ni nahodha msaidizi wa Simba inaelezwa kuwa mkwanja wake anaolipwa Simba kwa sasa ni chini ya milioni 5 ila anaanza kikosi cha kwanza ila wapo ambao wanapewa m 10 wanasugua benchi ndani ya kikosi.

"Unajua Tshabalala ni mchezaji mzuri na ana uwezo mkubwa, ambacho kinatokea ni kwamba analipwa mshahara chini ya laki milioni 5 halafu anachukuliwa kawaida kwa sababu ni mzawa sasa.

"Wapo wachezaji wa kigeni ambao ni (anawataja majina) hawa wanalipwa zaidi ya milioni 5 halafu hawapo kwenye mipango ya kocha na wengine walichukua mkwanja mrefu hawajacheza mchezo hata mmoja," ilieleza taarifa hiyo.

 Habari zinaeleza Tshabalala kwa sasa anahitaji mshahara zaidi ya milioni 8 na mkataba wake anahitaji ufanyiwe maboresho zaidi ya awali.

Meneja wa mchezaji huyo, Herry Mzozo amesema kuwa kipaumbele cha kwanza ni Simba na wakifika makubaliano basi mteja wake atasaini dili jipya.

Mkataba wake unaisha msimu 2020/2021 anakuwa mchezaji huru na inaelezwa kuwa timu zaidi ya tano zimempa ofa beki huyo ili kupata saini yake.

8 COMMENTS:

  1. Mnatengeneza story ili kuuza magazeti, ina hitaji mtu mwenye upeo wa juu kuwaelewa, anyway hongereni sana, ni mbinu ya kupata hela katika wakati huu wa biashara yenye ushindani. Mnatumia mianya mbalimbali kuwa fursa ya kujipatia viewers na wateja wa habari zenu, lakini nyuma ya pazia stori ipo tofauti na uhalisia. Moyo thabiti hauyumbishwi hovyo.

    ReplyDelete
  2. Doctor, that is mere opinions, no research no rights to speak.

    ReplyDelete
  3. Mkataba wa kila mchezaji ni makubaliano ya pande mbili bila kuangalia mwingine analipwaje. Kila mchezaji anapbana kushawishi na sio kuangalia mwenzangu analipwaje. Ukiona huridhiki achana na huo mkataba. Hazad madrid analipwa kiasi gani, anacheza? Acheni ujinga ninyi wachonganishi

    ReplyDelete
  4. hii 'blog' huwa inakera Sana, it's very partially and shallow. Jifunzeni kwa "Mwanaspoti"

    ReplyDelete
  5. Very shallow indeed, anasema analipwa mshahara chini ya "laki milioni 5", hii sijui ni sentensi ya mtu mwenye taaluma au la?

    ReplyDelete
  6. Badala ya kuandika matokeo ya Jana anaandika habari zisizoeleweka

    ReplyDelete
  7. Mbona mmeshupalia hii habari? Kwani mwenyewe hana mdomo? Inajulikana mmetumwa kucheza mind games za upande wa pili lakini simba imejipanga, hamtaweza. Kuleni tuu hizo hela za hao wapuuzi wanaowatuma

    ReplyDelete
  8. Chini ya laki milioni 5 indeed Makanjanja waliopo kwenye pay roll basi kuweni hata na weledi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic