April 19, 2021

 


WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa, amebainisha kwamba, leo Jumatatu, Simba na Tume ya Ushindani (FCC) watakutana ili kujadili hatima ya suala la uwekezaji ndani ya klabu hiyo.

Hayo yametokea mara baada ya waziri huyo kujibu swali bungeni aliloulizwa na Mbunge wa Jimbo la Mlalo, Tanga, Rashid Abdallah Shangazi alipoulizwa juu ya suala la uwekezaji ndani ya Simba.

 

Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohammed Dewji, aliandika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii kuonesha kuilalamikia FCC kuchelesha suala la mabadiliko ndani ya Simba.


Waziri Bashungwa alisema kuwa, Serikali imelitazama jambo la FCC na uwekezaji wa Simba, hivyo watafanya kila liwezekanalo ili jambo hilo kukamilika kwa haraka zaidi ili Simba waingie katika mfumo mzuri wa mabadiliko ya kiuendeshaji.


“Serikali tumelitizama jambo hili na tutalifanyia kazi ili Simba waweze kufanikisha jambo hili, hivyo Jumatatu Simba watakaa kikao na FCC ili kuendelea kuangalia watafanikisha vipi jambo hili la uwekezaji ndani ya Simba,” alisema Waziri Bashungwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic