April 20, 2021


 BAADA ya kipa wa Polisi Tanzania Mohamed Yusuph, kuokota mabao mawili kwenye nyavu zake, Saleh Ally,'Jembe' mchambuzi wa masuala ya michezo amesema kuwa kuna haja ya kipa huyo kuhojiwa na uongozi wa timu hiyo.

Polisi Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Malale Hamsini ilikubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Ushirika Moshi.

Mabao hayo kwenye mchezo wa ligi uliochezwa, Moshi Aprili 18 yalifungwa na mchezaji mmoja ambaye ni Jeremia Kisubi.

Ilikuwa ni dakika ya 16 Kisubi akiwa ndani ya 18 alimtungua kwa kichwa huru Yusuph baada ya kupokea pasi ndefu kutoka kwa Salum Kimenya.

Bao la pili ilikuwa dakika ya 80 kwa mfungaji yuleyule Kisubi kumtungua tena kipa huyo kwa kichwa akiwa ndani ya 18 akitumia pasi ya Ezekia Mwashilindi ambaye naye alipiga pasi hiyo kupitia mpira uliokufa akiwa nje ya 18.

Ni Idd Moby wa Polisi Tanzania ambaye alipachika bao la kufutia machozi ilikuwa dakika ya 34 naye pia ilikuwa kwa kichwa akiwa ndani ya 18 kwa pasi ya Daruesh Saliboko.

Matokeo hayo yameifanya Polisi Tanzania kubaki na pointi 34 ikiwa nafasi ya 7 huku Prisons ikifikisha jumla ya pointi 34 ipo nafasi ya 9.

Jembe amesema:"Angalia vizuri mabao mawili ya Prisons dhidi ya Polisi Tanzania yamefungwa na Jeremiah Juma Ally. Lakini Polisi wamhoji kidogo kipa wao, uzembe huu ni wa kiwango cha lami au kuna nini?," .

4 COMMENTS:

  1. Siamini kama kuna waandishi utopolo kama wewe yaani unaongea kama shabiki wa mtaani mbona husemi kipa wa biashara ahojiwe kwa goli la kizembe alilofungwa

    ReplyDelete
  2. Saleh Jembe wamedukua account yako. Omba radhi. Uliloliandika limekosa weledi wa kiandishi.Magoli yote matatu ,mbili dhidi ya Polisi na moja dhidi ys Prisons ni makosa ya kawaida ya magolikipa.
    Umeangalia mechi yote .Kuna faulo iliyopigwa na Salum Kimenya na kipa Mohamed Yusuf akaipangua na kuwa kona. Ilikuwa save ya kimataifa.
    Waachie mashabiki maandazi ndio waje na tuhuma kama hizo wewe unaheshimika kama mwandishi nguli.Omba msamaha umeteleza.

    ReplyDelete
  3. Uambie pia uongozi wa Manchester United wamuhoji kipa wao kwa uzembe aliouonesha kwenye mechi yao na Brighton maana nae alitunguliwa goli la kichwa na pia alikuwa anafanya uzembe mwingi wa kutoka golini bila mpangilio sasa sijui nae alikuwa ana ajenda gani ya siri dhidi ya timu yake

    ReplyDelete
  4. Mabao yalifungwa na Jeremiah kisubi golikipa wa prison?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic