JOSE Mourinho ametimuliwa ndani ya kikosi cha Tottenham zikiwa zimesalia siku tano kabla ya timu hiyo haijacheza Fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya Manchester United.
Kutimuliwa kwa kocha kocha huyo kumetokana na mwendo mbovu wa timu hiyo msimu huu ikiwa haina uhakika wa kuingia ndani ya nne bora.
Timu hiyo kwenye Ligi Kuu England ipo nafasi ya saba imekusanya pointi 50 baada ya kucheza jumla ya mechi 32 na ina mechi sita mkononi kumaliza msimu huu wa 2020/21.
Kocha huyo aliibuka ndani ya Spurs Novemba 2019 kwa matumaini makubwa ya kufanya vizuri akichukua mikoba ya Mauricio Pochettino na alisaini mkataba wa miaka minne ila amekiongoza kikosi hicho kwa miezi 17 na kutimuliwa mazima.
Mourinho ameifikisha timu hiyo hatua ya Fainali ya Carabao ila ametolewa kwenye FA hatua ya nusu fanali na hajashinda taji lolote lile na inakuwa ni mara yake ya tatu kuweza kutimuliwa ikiwa ni Chelsea, Manchester United na sasa Tottenham.
0 COMMENTS:
Post a Comment