April 11, 2021


IMEELEZWA kuwa kinachomsumbua kipa namba moja wa Azam FC, David Kissu ni matatizo ya kisaikolojia jambo ambalo linamfanya ashindwe kuonyesha ubora ambao alianza nao.

Habari kutoka kwa mtu wa karibu wa Kissu zimeeleza kuwa matatizo ambayo amekuwa akikutana nayo Kissu yamemfanya aporomoke ghafla kiwango chake jambo lililofanya nafasi yake ichukuliwe na Mathias Kigonya.

Kissu ambaye ni ingizo jipya ndani ya Azam FC akitokea Klabu ya Gor Mahia alianza vizuri mzunguko wa kwanza ambapo timu hiyo ikiwa chini ya Arstica Cioaba ilicheza jumla ya mechi 7 bila kupoteza na ikawa ni namba moja.

Ilipoteza mchezo wa kwanza msimu wa 2020/21 kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar jambo ambalo liliwafanya mabosi wa Azam FC kuanza kufikiria namna ya kuboresha safu ya ulinzi pamoja na mlinda mlango.

Mtu huyo amesema:"Kissu ni chaguo namba moja kwa makocha pale Azam FC ila kinachomsumbua ni matatizo ya kisaikolojia bado hajakaa sawa akikamilisha mambo yake nina amini kwamba atarudi kwenye ubora wake,".

Hivi karibuni, Kocha Msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati alisema kuwa makipa wote wa Azam FC ni bora ila kuna wakati wanafanya makosa ambayo yanatokana na sababu mbalimbali.

"Makipa wote Azam ni wazuri ila kuna wakati wanafanya makosa ambayo yanawafanya wafungwe na tunayafanyia kazi," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic