April 11, 2021


 HEMED Morroco, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa watarekebisha makosa yao na kupata ushindi mbele ya Nkana FC kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho utakaochezwa leo Aprili 11 Jumapili dhidi ya Nkana.

 Wawakilishi hao wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika, watakuwa Uwanja wa Levy Mwanawasa, Zambia, ukiwa ni mchezo wa nne wa michuano hiyo hatua ya makundi ambapo timu hizo zipo Kundi D.

 

Katika mchezo uliopita baina ya timu hizo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar, Namungo ilikubali kichapo cha bao 1-0.

 

Akizungumza na Saleh JembeMorocco amesema: “Hii ni nafasi nyingine kwetu kupambana kwa ajili ya kutetea heshima ya taifa letu, tumewapa maandalizi ya kutosha vijana wetu na kufanya marekebisho ya mapungufu tuliyoyabaini katika michezo iliyopita.

 

“Kila mchezo kwetu ni nafasi ya kujifunza kwa kuwa hii ni mara ya kwanza kushiriki mashindano haya makubwa, hivyo tutapambana kuona tunapata matokeo mazuri, kama walitufunga kwetu basi na sisi tunaweza kupata matokeo bora kwao," .


Katika kundi D, Namungo haijakusanya pointi baada ya kupoteza mechi zote tatu na jana ilikwea pipa kuibukia Zambia ambapo leo itakuwa uwanjani kupeperusha Bendera ya Tanzania.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic