April 10, 2021

 


HABIB Kondo, Kocha Msaidizi wa Klabu ya KMC amesema kuwa hawawaogopi wapinzani wao Yanga bali wanawaheshimu.

Leo KMC iliyo nafasi ya tano na pointi 35 baada ya kucheza jumla ya mechi 24 inakutana na Yanga iliyo nafasi ya kwanza na pointi 50 baada ya kucheza jumla ya mechi 23.

Kondo ameweka wazi kuwa wanatambua mchezo wa leo utakuwa na ushindani mkubwa ila baada ya dakika 90 kila kitu kitakuwa wazi.

"Hatuwaogopi Yanga ila tunawaheshimu kwa sababu ni timu bora na inaongoza ligi, kwa maandalizi ambayo tumefanya tunaamini tutapata matokeo.

"Kuhusu namna ambavyo tutafanya kupata ushindi hilo litajulikana uwanjani, mbinu yetu hatuwezi kuiweka wazi kwa kuwa wanaweza kuifanyia kazi,".

Walipokutana mzunguko wa kwanza , Uwanja wa CCM Kirumbaubao ulisoma KMC 1-2 Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic