April 10, 2021


 BAADA ya kukamilisha mchezo wao wa mwisho hatua ya makundi katika Ligi ya Mabingwa Afrika, wawakilishi wa Tanzania, Simba wameanza safari ya kurejea Tanzania kupitia Dubai.

Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes kilipoteza mchezo wake wa jana Aprili 9, kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Al Ahly.

Licha ya kupoteza mchezo huo ugenini, Simba imeweza kutinga hatua ya robo fainali kwa sababu kabla ya mchezo huo ilikuwa imefanikiwa kukata tiketi ya kushiriki hatua ya robo fainali.

Al Ahly imelipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 ilipotua Bongo, ambapo mfungaji wa bao hilo alikuwa ni Luis Miquissone.

Ushindi wao wa mabao 4-1 dhidi ya AS Vita ambayo jana ilishinda mabao 3-1 dhidi ya Al Merrikh uliwapa nafasi Simba kufikisha jumla ya pointi 13 ambazo hazijafikiwa na Al Ahly ambao kwa sasa wana pointi 11.

Kwenye kundi A ni Simba yenye pointi 13 na Al Ahly zimetinga hatua ya robo fainali huku AS Vita yenye pointi saba na Al Merrikh yenye pointi mbili zikiishia hatua ya makundi.

Simba inarejea Bongo kwa ajili ya kuendelea na mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho ambapo ipo hatua ya 16 bora na ina kazi ya kutetea mataji yote hayo mawili.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic