April 17, 2021

 





FT: Yanga 1-0 Biashara United 
Uwanja wa Mkapa

Yanga imesepa na pointi tatu mbele ya Biashara United 
Dakika ya 90+1 Sarpong anaingia anatoka Kaseke 
Zinaongezwa dakika 4
Dakika ya 90 Shikalo anaanzisha mashambulizi 
Dakika ya 87 Kaseke anafanya jaribio linaokolewa na kipa Mgore 
Dakika ya 83 Nchimbi anaingia anatoka Yacouba 
Dakika ya 83 Lenny Kissu anaonyeshwa kadi ya njano 
Dakika ya 81 Adeyum anafanya jaribio linaokolewa na Mgore
Dakika ya 79 Kibwana Shomari anachezewa faulo 
Dakika ya 76, Saido Ntibanzokiza anatoka anaingia  Haruna Niyonzima 
Dakika ya 75 Job anachezewa faulo 
Dakika ya 70 Kaseke anapewa huduma ya kwanza 
Dakika ya 68 Saido anafanya jaribio linakwenda nje kidogo ya lango 
Dakika ya 64 Ally Kombo anaonyeshwa kadi ya njano 
Dakika ya 58, Gooooooal Yacouba pasi ya Adeyum
Dakika ya 57 Job anafanyiwa faulo na Zigah
Dakika ya 55 Kaseke anakuwa eneo la kuotea
Dakika ya 54 Adeyum anafanya jaribio linaokolewa na mabeki wa Biashara United 
Dakika ya 53, Mgore anaonyeshwa kadi ya njano 
Dakika ya 51 Mgore anapewa huduma ya kwanza 
Dakika ya 50 Carinhos anapiga kona haileti matunda 
Dakika ya 48 Yacouba anafanya jaribio linakwenda nje ya lango 
Dakika ya 46 Judika anafanya jaribio linakwenda nje ya lango 
Kipindi cha pili kimeanza 
Mapumziko 
UWANJA wa Mkapa
Ligi Kuu Bara 

Yanga 0-0 Biashara United 

Dakika ya 45+2 Carinhos anapiga kona ya pili inakuwa sawa na Biashara United zote hazijaleta matunda

Zinaongezwa dakika 4

Dakika ya 45 Biashara United wanaanza kona fupi inaokolewa 

Dakika ya 44 Mafie anapeleka mashambulizi kwa Shikalo yanaokolewa na Adeyum 

Dakika ya 43 Mgore anaokoa hatari 

Dakika ya 41 Kisinda anapeleka mashambulizi kwa Mgore

Dakika ya 38 Zigah anapewa huduma ya Kwanza baada ya kugongana na Dickson Job 

Dakika ya 36 Carinhos anapiga faulo inaishia mikononi mwa Mgore

Dakika ya 35 Carinhos anafanya jaribio linakwenda mikononi mwa Mgore

Dakika ya 34 Mafie anaotea

Dakika ya 31 Mafie anafanya jaribio linaokolewa na Shikalo

Dakika 31 Yanga wanapata kona inapigwa na Carinhos 

Dakika ya 30, Faulo ya Carinhos inakwenda kugonga nyavu za nje

Dakika ya 28 Kaseke anachezewa faulo nje kidogo ya 18 anapewa jukumu la kupiga Carinhos 

Dakika ya 27, Kaseke anachezewa faulo,Shikalo anaokoa hatari ndani ya eneo lake la 18.

Dakika ya 25 Kisinda anachezewa faulo 

Dakika ya 23, Tonombe anapiga shuti nje ya lango

Dakika ya 21 mchezaji wa Biashara United anapewa huduma ya kwanza

Dakika ya 18 Mangalo anaokoa hatari iliyokuwa miguuni mwa Kaseke ndani ya 18

Dakika ya 15 Kisinda anafanya jaribio linaokolewa na Mgore

Dakika ya 14, Carinhos anafanya jaribio akiwa nje ya 18 kwa pasi ya Saido, Kaseke naye anafanya jaribio yote yanaokolewa.

Dakika ya 12 Carinhos anapeleka kwa Saido Ntibanzokiza ngoma inaanuliwa inarudi kwa Yanga

Dakika ya 9 Kisinda anacheza faulo kwa Yanga baada ya kunawa mpira

Dakika ya 8 Yacouba anafanya jaribio linaokolewa na Mgore

Dakika ya 4 Kaseke anapiga shuti linakwenda nje ya lango 

Dakika ya 3 Zinga anapeleka mashambulizi yanaokolewa

1 COMMENTS:

  1. Wache wajifurahishe lakiniwa hali ya Mnyama ilivo, ubingwa wausahau kabiss

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic