CLATOUS Chama, mwamba wa Lusaka ambaye ametupia mabao 7 pamoja na Meddie Kagere mwenye mabao 11, idadi ya mabao ambayo wamefunga ni sawa na yale ambayo yamefungwa na wapinzani wao Mwadui FC.
Jumla ya mabao ya nyota hao wawili ni 18 wakiwa wamecheza jumla ya mechi 21 huku safu ya ushambuliaji ya Mwadui FC ikiwa imefunga mabao 18 baada ya kucheza jumla ya mabao 25.
Leo, Uwanja wa Kambarage, Shinyanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao utakuwa ni mzunguko wa pili kwa sababu walikutana Uwanja wa Uhuru na ubao ulisoma Simba 5-0 Mwadui FC, timu zote mbili zitakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu.
Utakuwa ni mchezo wa ushindani ndani ya dakika 90 kwa kuwa Mwadui FC inapambana kujinasua kwenye hatari ya kushuka daraja ikiwa nafasi ya 18 na pointi 16 huku Simba ikipambana kutetea taji la ligi, ina pointi 49 ipo nafasi ya tatu.
Kocha Mkuu wa Simba, Dider Gomes amesema kuwa kikubwa ambacho anahitaji kwenye mechi zake zote ni pointi tatu muhimu.
0 COMMENTS:
Post a Comment