MANCHESTER United inayonolewa na Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solskjaer, leo Aprili 18 imetakata Uwanja wa Old Trafford kwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Burnley.
Mchezo huo wa Ligi Kuu England ulikuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika 90 ambapo United walipiga jumla ya mashuti 17 na Burnley 10 kati ya hayo 9 ya United yalilenga lango na matatu kwa Burnley yalilenga lango.
Ni Mason Greenwood alitupia mabao mawili alianza la ufunguzi dakika ya 48 na la pili alipachika dakika ya 84 na la tatu ni mali ya Edinson Cavan alitupia bao hilo dakika ya 90+3.
Kwa Burnley ni James Tarkowski alipachika bao dakika ya 50 na kuwafanya United wazidi kupambana mpaka kusepa na pointi tatu mazima.
United inafikisha pointi 66 ipo nafasi ya pili na Burnley ipo nafasi ya 17 na pointi 33 zote zimecheza mechi 32.
0 COMMENTS:
Post a Comment