April 29, 2021


BAADA ya kete yake ya kwanza akiwa kwenye benchi la ufundi Kocha Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi kushushudia ubao ukisoma Yanga 0-1 Azam FC amekabidhiwa dakika 630 za moto ambazo ni mechi 7 ndani ya Ligi Kuu Bara zenye alama 21.

Nabi raia wa Tunisia amekabidhiwa mikoba ya Cedric Kaze ambaye alichimbishwa kazi kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni matokeo mabovu ya timu hiyo alianza mechi ya kwanza kwa kukaribishwa kwa kupoteza mbele ya Azam FC.

Kigongo chake kijacho kwenye ligi ni Mei 8, itakuwa dhidi ya  Simba ambapo itakuwa ni dabi yake ya kwanza mchezo wao uliopita ubao ulisoma Yanga 1-1 Simba.

Kisha Mei 15, itakuwa ni Namungo v Yanga walipokutana mzunguko wa kwanza ubao ulisoma Yanga 1-1 Namungo. Mei 19 ana kazi ya kusaka ushindi mbele ya JKT Tanzania walipokutana kwa Mkapa ubao ulisoma Yanga 1-0 JKT Tanzania

Juni 19 ana kazi mbele ya Ruvu Shooting ambapo mzunguko wa kwanza ubao ulisoma Yanga 2-1 Ruvu Shooting. Juni 22 atakuwa na Mwadui FC ambao mzunguko wa kwanza ubao ulisoma Mwadui 5-0 Simba. Julai 8, itakuwa mbele ya Ihefu huku rekodi zikionyesha kwamba mchezo uliopita ubao ulisoma Ihefu 0-3 Yanga.

Nabi ikiwa bado atakuwa hajachimbishwa basi atakamilisha kete yake ya mwisho ya dakika 630 mbele ya Dodoma Jiji, Julai 11, mchezo wa mzunguko wa kwanza ubao ulisoma Yanga 3-1 Dodoma Jiji.

3 COMMENTS:

  1. Wewe mwandishi wewe! Simba anaingiaje hapo kwenye mechi ya Mwadui na Yanga? Matokeo yalikua Mwadui 0 - 5 Yanga na sio Mwadui 5 - 0 Simba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umakini mdogo, bora liende

      Delete
    2. Watu wanaiota simba tu,ata kocha huyo wa yanga kwenye mkutano wake alitaha simba badla ya yanga.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic