April 21, 2021


 MSHAMBULIAJI mzawa ndani ya Klabu ya Yanga, Ditram Nchimbi amesema kuwa hakumbuki mara ya mwisho kufunga ilikuwa lini katika mechi zake za ushindani.

Nyota huyo alipitisha mwaka mzima bila kufunga kwenye mechi za ushindani ila aliweza kufunga jana Aprili 20 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Gwambina FC.

Kwenye mchezo huo Yanga ilishinda mabao 3-1 kisha ilisepa na pointi tatu jumlajumla. Mabao mengine yalifungwa na Bakari Mwamnyeto na Saido Ntibanzokiza ambaye alipofunga aliomba kufanyiwa mabadiliko na Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi.

Bao la Gwambina FC lilifungwa na Jimsone Mwanuke ambaye alipachika bao hilo akiwa nje ya 18 likamshinda mlinda mlango, Faroukh Shikalo.

Nchimbi amesema:"Mara ya mwisho sikumbuki ilikuwa lini nimefunga ila nimefurahi kuona kwamba nimefunga kwa kuwa ushindi ni jambo la msingi na tumefurahi," amesema.

Yanga ikiwa imefunga mabao 41 yeye ametupia bao moja na ametoa pasi mbili za bao.

6 COMMENTS:

  1. Ukweli ni kwamba kwangu Mimi hata Kama hafungi Ana uwezo wa mikimbio ya kusaidia Timu kuliko hata wanaofunga ,huo ndiyo ukweli ila baadhi yenu mnamwogopa hamtaki acheze against you so mnajenga mazingira ya kumtoa na kuwafanya Yanga wasimwamini ,mpate unafuhu Yanga kwa Sasa hatuna Molinga na mechi ijayo ataanza mbele Sarpong,Yakuba,Nchimbi naTuisila the only mido atakuwa Mukoko mjiandae

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kinyago chako mwenyewe alafu kinakutishia,ha ha ha ha ha ha kamuulize Walter bwalya atakupa majibu brother.the time will tell Acha kila mtu ashinde mechi zake alafu mwisho wa siku tukutane kwenye jedwali.

      Delete
  2. Kwenye soka jukumu kubwa la striker ni kufunga lingine ni kutoa assist.... Kama mnapima strikers wenu kwa mikimbio basi subirini mwisho wa siku muone mtakachovuna

    ReplyDelete
  3. Hahahaa.... Mikimbio isiyo na faida

    ReplyDelete
  4. Nchimbi atabaki kuwa juu mawinguni

    ReplyDelete
  5. Mikia fc wanamjua huyo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic