April 24, 2021



LEO Aprili 24 Simba ikiwa na kazi ya kusaka pointi tatu muhimu mbele ya Gwambina FC, mchezo wa ligi utakaochezwa Uwanja wa Gwambina Complex itawakosa nyota wake 10 kutokana na sababu mbalimbali.

Nyota hao ambao watakosekana leo ni pamoja na Luis Miquissone ambaye ni kiungo mshambuliaji, Taddeo Lwanga ambaye ni kiungo mkabaji na beki wa kati Pascal Wawa hawa wataukosa mchezo kwa sababu wana kadi tatu za njano.

Kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar, uliochezwa Uwanja wa Kaitaba wakati ubao ukisoma Kagera Sugar 0-2 Simba nyota hao kila mmoja alionyeshwa kadi moja ya njano na kufanya wafikishe jumla kadi tatu kwa kila mmoja.


Mbali na nyota hao watatu pia kiungo Francis Kahata yeye anaingia kwenye orodha ya watakaokosa mchezo wa leo licha ya kuwa na kikosi hicho kwa sababu jina lake lipo kwa wachezaji wanaoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na Simba ipo hatua ya robo fainali.

Wengine ambao wanatarajia kuukosa mchezo wa leo ni Kiungo Said Ndemla, Ibrahim Ajibu, Miraj Athuman hawa kwa sasa bado hawajawa fiti kuanza kupambana kikosi cha kwanza pamoja na kipa namba tatu, Ally Salim.

Beki wa kushoto Gadiel Michael na mshkaji wake David Kameta, 'Duchu' ambaye ni beki wa pembeni bado wanapambana kuingia kikosi cha kwanza hawana uhakika wa kuanza leo.


2 COMMENTS:

  1. Mechi ya kesho licha ya udhaifu wa Gwambina lakini niwatahadharishe tu viongozi na wachezaji na Benchi la Simba kuwa mechi hiyo itajaa fitina la kila aina. Tayari fitina zimeshaanza kwenye mitandao ya kijamii ili kuitoa Simba mchezoni. Suala la Madai ya Asante kwasi ni la kisiasa zaidi ili kuitoa simba mchezoni kwenye mechi ya jumamosi. Timing ama muda wa taarifa hizi sikucha chache kabla ya mechi ya simba na Gwambina kwa simba kuelekea kushika usukani wa ligi unaona kabisa kuwa kuna mchezo mchafu wa kuwatibua simba kutoka nje ya mchezo. Ilitokea hivi hivi kwa kichuya wakati samba iliporudi kutoka kwenye mechi za kimataifa na wakati ule kwa kiasi fulani watengeneza fitina hawa walifanikwa kuiyumbisha simba kidogo kwenye ligi. Kwa hivyo tunawaomba viongozi wa simba kuwa makini zaidi kipindi hiki hasa kwenye mechi ya kesho. GWAMBINA kama Mwadui na hasa kwakuwa wametoka Daresalam kucheza na Yanga si ajabu watakuwa wameahidiwa kitu na Yanga ili kuitubulia simba. Na inawezekana kabisa hata baadhi ya watu wa Yanga kuambatana na msafara wa Gwambina ili kuja kujaribu kuharibu matokeo ya simba. Kwa hivyo sio mechi ya kuichukulia poa kwa simba hata kidogo.Gwambina watajilinda zaidi kuanzia mwanzo wa mchezo.Hivyo benchi la ufundi la simba lazima liwe na mipango kazi ya kulazimisha goli la mapema ili kuwafungua Gwambina. Simba wasije kurejea kufanya makosa waliofanaya zidi ya mwadui ya kuwapa kujiamini mwadui kila mechi ilipokuwa ikiendelea bila simba kupata goli.

    ReplyDelete
  2. Wajihadhari na kadi za kutengenezwa hawa mayai viza fc ni tatizo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic