April 12, 2021



VIUNGO wawili wa kikosi cha Yanga, Saido Ntibanzokiza na Tuisila Kisinda chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi wamepewa mikoba ya kiungo Muangola Carlos Carlinhos.

Ndani ya kikosi cha Yanga, Carlinhos alikuwa anaaminika kwa kupiga mipira iliyokufa ikiwa ni kona pamoja na faulo na ana pasi mbili za mabao ambazo zilitokana na mipira hiyo ila juzi alikosekana kwenye mchezo wa ligi dhidi ya KMC jambo lililofanya mikoba yake kuwa mikononi mwa Kisinda na Saido.

Wakati ubao wa Uwanja wa Mkapa, ukisoma Yanga 1-1 KMC, Saido alipiga jumla ya faulo 10 na moja kati ya hiyo ilileta bao lilifungwa na Yacouba Songne dakika ya 46.

Kwa upande wa Kisinda yeye alipiga jumla ya kona 4 ambazo zote zilikuwa zinaanuliwa jumlajumla anga za KMC na Andrew Vincent, ‘Dante’ ambaye alikuwa kwenye ubora wake.  

Mwambusi amesema kuwa aliamua kuwabadilishia majukumu wachezaji wake kwa sababu anahitaji kutengeneza muunganiko mzuri katika kikosi hicho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic