JOASH Onyango beki wa kati wa Simba chaguo namba moja la Kocha Mkuu, Didier Gomes, raia wa Ufaransa amesema kuwa wataendelea kupambana kuzuia kutokufungwa kwenye mechi zote ambazo watacheza.
Leo Aprili 14, Simba ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara. Imetoka kumalizana na Al Ahly katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.
Timu hizo mbili zote zimetinga hatua ya robo fainali wakitokea kundi A ambapo kinara ni Simba mwenye pointi 13 na Al Ahly ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 11.
Akizungumza na Saleh Jembe, Onyango ambaye kwenye ligi ametupia bao moja amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi zao zote na watapambana ili wasifungwe.
"Tumemaliza mashindano ya kimataifa hatua ya kwanza na tunaamini kuna hatua nyingine ambayo inakuja tupo tayari kwa ajili ya robo fainali na tutapambana ili tupate matokeo mazuri kwa kulinda lango ili tusifungwe.
"Kwenye ligi pia tunazidi kupambana ili kupata matokeo mazuri, kila kitu kinawezekana na tutazidi kushindana kila wakati," .
0 COMMENTS:
Post a Comment