BEKI wa kati wa Simba, Pascal Wawa raia wa Ivory Coast amesema kuwa licha ya kushiriki mashindano ya kmataifa bado wana hesabu za kufanya vizuri kwenye ligi pia.
Beki huyo amesema kuwa bado nao wana mipango kwenye ligi kwa kuwa hawakucheza kutokana na kushiriki mashindano ya kimataifa.
Ikiwa imetinga hatua ya robo fainali ilikamilisha hatua ya makundi Aprili 9 kwa kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Al Ahly.
Wawa amesema kuwa kitendo cha wao kuwa bize na michuano ya kimataifa isiwe sababu ya wapinzani kuona urahisi kwa kuweza kutwaa ubingwa wa ligi kuu kwa kuwa hata wao bado wana malengo ya msingi.
“Unajua hii michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika imekuwa ni migumu sana lakini kadiri tunavyopiga hatua ndiyo matarajio na malengo yetu yanazidi kuwa makubwa maana tumefikia kwenda kucheza robo fainali lakini malengo tufike nusu fainali.
“Nadhani kuwa bize huku kusiwe sababu ya wengine kuchukulia kuwa ni sehemu ya kuweza kusahau kuwa bado kuna mechi za ligi kwa sababu licha ya kushiriki Ligi ya Mabingwa bado tunahitaji kushinda ubingwa wa ndani wa ligi hivyo haiwezi kuwa jambo rahisi,” amesema Wawa.
Kwenye msimamo Simba ipo nafasi ya tatu na pointi 46 baada ya kucheza mechi 20 huku nafasi ya kwanza ikiwa mikononi mwa Yanga yenye pointi 51 baada ya kucheza mechi 24.
0 COMMENTS:
Post a Comment