BARCELONA imekubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya wapinzani wao wakubwa Real Madrid katika mchezo wa La Liga maarufu kama El Clasico.
Ni Karim Benzema alianza kutikisa nyavu za Barcelona ikiwa na mshambuliaji wao namba moja Lionel Messi dakika ya 13 na bao la pili lilifungwa na Toni Kroos dk ya 28 na kuwafanya waende mapumziko wakiongoza.
Barcelona ilipata bao la kufuta machozi dakika ya 60 kupitia kwa Oscar Mingueza ilikuwa ni Uwanja wa Alfredo Di Stefano ambapo nyota wa Real Madrid Casemiro alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 90.
Ushindi huo unaifanya Madrid kufikisha alama 66 ikiwa nafasi ya kwanza na Barcelona nafasi ya tatu ilibaki na pointi 65 zote zimecheza mechi 30.
0 COMMENTS:
Post a Comment