April 25, 2021


BAADA ya kuwa na tetesi kwamba beki wa kushoto wa Simba, Mohamed Hussein ameingia kwenye rada za watani wa jadi, Yanga, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ameomba uongozi umalizana na mchezaji huyo mapema kabla hajasepa huku akiweka wazi kwamba watamruhusu mchezaji huyo kwenda nje ya nchi na sio katika timu nyingine.

Ndani ya Simba, Zimbwe mkataba wake umebaki miezi miwili ambapo bado hajaongeza dili jingine licha ya kuwa kwenye mazungumzo na mabosi hao.

Kupitia ukurasa wa Instagrma wa Haji Manara ameandika namna hii:-"Wewe ndio mchezaji unaeimbwa zaidi na wasanii wa Bongo kwa mahaba yao kwako.

Wewe ni Captain, (nahodha) wetu unaependwa ná kila mmoja ndani ya Simba.

"Hii ni timu ya maisha yako na hapa ndio umekulia na kupata jina lako. Mimi na wewe tuliingia pamoja msimu wa 2014 ni mate wangu. Tumetoka mbali na hii klabu. Tunayajua mengi mazuri na changamoto za klabu hii.

"Tumetengeneza bond kubwa na Simba, hakuna thamani ya pesa itakayotufanya tuondoke Simba kwenda klabu nyingine ya Tanzania.

"Wanasimba wamenituma nikwambie hadharani, umalizane haraka na uongozi wa klabu kuhusu usajili wako na hawatakubali kukupoteza kwa namna yoyote ile. Sanasana watakuruhusu uende nje ya nchi hii.

"Don’t forget, (usisahau) wanaokushawishi leo walikudhihaki jana, usikubali kuiacha team ambayo inakuandaa uwe legendary wake na inayokupa furaha kisha ukacheze team usiyoishabikia eti kwa sababu ya visumuni vya kupita.

"Furaha na amani ya moyo inazidi rupia za kupita !Babra, (Gonzalez) boss wangu, nchi haitatuelewa Zimbwe akiondoka 

"Huyu ni Mtoto wa Simba, limalize hili tuendelee kuonyesha nini Simba inadhamiria katika muendelezo wa ukubwa wake!

"Naombeni tutangeneze hashtag yoyote ya kumtaka Mohammed Hussein Zimbwe Junior aongeze mkataba Simba," .

16 COMMENTS:

  1. Manara sa nyingine anaongea ujinga, kama Zimbwe anataka kwenda yanga wamwache, yeye mwenyewe anajuanipi ni klabu bora Tanzania. Hizo kelele ni za kutengenezwa na meneja wake na magazeti ili apate mkataba mnono. Simba ni kubwa kuliko mchezaji mmojammoja.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa simba shabalala akiamua kuondoka sawa mbona ligi imejaa mafulbeck wengi wazuri haina haja hata simba kwenda nje.Simba kama CCM unakuwa bora ukiwa ndani ya chama ukitoka ni wa kawaida sana.

      Delete
  2. No point captured,,, mpeni helaa sio maneno ya kwenye kanga

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yanga wana hela ya kumpa mchezaji yeyote wa Simba..Utopolo wanatakiwa wafikirie namna gani watakavyoenda kimataifa bila kupitia jasho la Simba...Sio kila wakiona mkataba wa wachezaji Simba mfano Zimbwe unakaribia kuisha wanaanzisha maneno kuwa wanataka msjili.ilikuwa hivyo pia kwa Chama

      Delete
    2. We au mama yako mna hela?

      Delete
    3. wewe Zeph ni mume wako na mama yako ndiyo hawana hela!

      Delete
  3. Rodrick kwa hili sikuungi mkono.Tshabalala ni mchezaji muhimu hivyo inahitajika juhudi kumbakisha. Ukiwa na maamuzi ya hasira huwezi kubaki na mchezaji.Kama tunawalipa wachezaji wa kigeni?Why not Tshabalala ambaye anacheza kwa moyo.Angalia jana alivyoshangilia goli alilofunga.Mapenzi yake kwa Simba yaenziwe na kupewa shukurani kwa kazi nzuri.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hapa ni mchezo unachezwa na meneja wake na magazeti lazima utambue hilo kwanza.
      Wamesema yanga wanataka kumpa milioni 150 huo ni uwongo halafu meneja wake anasema wana ofa tatu nje ya nchi yote hayo ni kuwapa presha Simba ili watoe pesa nyingi manara kama sehemu ya menejimenti ya Simba alipaswa kukaa kimya.
      Kwa milioni hamsini unapata beki mzuri kabisa wengine wanaonekana wazuri kutokana na chemistry ya wachezaji iliyotengenezwa ukiwatoa hapo hamna kitu ndio maana hata stars uliona aliwekwa benchi.
      Ni kawaida ya mameneja na magazeti kufanya hivi kila mkataba unapoisha sasa hivi hawazungumzii Mkude sababu amepoteza namba kwenye kikosi bila hivyo ungesikia maneno kibao.

      Delete
  4. Mikia fc mnapenda kupigwa kila wakati mkituhusisha.. hehe

    ReplyDelete
  5. Rodrick hiyo ni biashara. Demand and supply determines the market.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni biashara iliyojaa madalali ndio maana naipinga, ana haki ya kupewa mkataba mzuri ila sio kwa stahili wanayotumia hao madalali

      Delete
  6. Nilitaka tukubaliane kwamba ana haki ya kupewa mkataba mzuri Tshabalala akichezea Simba anajituma haswa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ana haki ya kupewa mkataba mzuri tatizo kuna madalali wanaanza kutishia nyau

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic