April 15, 2021


WAKATI Simba inaingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa  Afrika kwa mara ya kwanza ikiivua Zamalek ubingwa wa Afrika, asilimia 95 ya kikosi chake kilikuwa ni cha wazawa.

Hii ilikuwa ni mwaka 2003, Simba ilicheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Zamalek kwenye Uwanja wa Taifa (sasa Uwanja wa Uhuru) na kuibuka na ushindi wa bao 1-0. Bao hilo lilifungwa na Emmanuel Gabriel “Batigol” ambaye alipokea krosi murua ya Ulimboka Mwakingwe.

Baada ya hapo, Simba wakasafiri kwenda Cairo, Misri na gumzo kubwa likawa kwamba watapoteza na zikiwa chache ni bao tano. Kumbuka, wakati huo Zamalek licha ya kuwa mabingwa wa Afrika, walikuwa ndiyo timu bora ya Bara la Afrika.


Mechi haikuwa nyepesi, Simba pamoja na kuwa na James Siang’a, pia walilazimika kuongeza nguvu ya makocha wengine kama Talib Hilal ambaye alisafiri kutoka nchini Oman kwenda kuungana na kikosi cha Simba.


Haikuwa mechi nyepesi, mwisho ikaisha Simba kulala kwa bao 1-0, likawa suala la mikwaju ya penalti, Kaseja akapangua penalti na Christopher Alex Massawe akamaliza kazi kwa kufunga mkwaju wa mwisho.

Nimeanzia mbali kidogo, lakini nilitaka kukupa picha tu kabla ya kuuliza maswali yangu wakati ukisoma makala haya nawe unaweza ukajiuliza mambo kadhaa na kupata kitu cha kujifunza, hiyo ndiyo nia yangu hasa.

Nimeizungumzia Simba ya mwaka 2003, lakini hata ningeizungumzia ile ya mwaka 1993 iliyoingia fainali ya Kombe la Caf, zaidi ungezungumzia wazawa wengi kama Hussein Marsha, George Magere Masatu, Edward Chumila na wengine wengi ambao walifanya vema wakati huo.

Simba sasa ndiyo timu inafanya vizuri zaidi katika michuano ya kimataifa kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Kwa kifupi niseme hivi, hata TP Mazembe na AS Vita, wababe hawa wa DR Congo, hawako vizuri kama Simba kwa msimu huu.

Wakati Simba ikiwa na mwendo bora kama huo, furaha na faraja ni kubwa kwa Watanzania kwa kuwa ni Simba ya Tanzania. Lakini mimi nawaza tofauti, kikosi cha Simba kama utakipanga kama si nusu kwa nusu, basi zaidi ya nusu, wanaotegemewa watakuwa ni wachezaji wa kigeni.

Bado ninaweza kusema si jambo baya sana lakini bado ni baya, maana inapendeza zaidi kuona timu inafanya vema zaidi ikiwa na wachezaji wengi zaidi wazawa.

Tunakubali uwepo wa wageni kama sehemu ya kukuza mpira wetu, mnaweza kuwa na timu bora ya taifa kutokana na kuwa na timu imara. Timu zinapokuwa na wazawa wengi na zinafanya vema na hasa kimataifa, basi mna nafasi ya kufanya vizuri zaidi kupitia timu ya taifa.

Hauwezi kuwalaumu Simba, umeona mara kadhaa wamejaribu kuwachukua wachezaji wazawa, mfano mzuri washambulizi ambao waliamini watafanya vema na waliwapa nafasi lakini mwisho wakawaangusha, mfano mzuri ni Adam Salamba  Na baadaye Charles Ilamfya ambaye pia alishindwa kabisa.

Wakati mwingine najiuliza, hivi sisi Tanzania hatuna hata mchezaji mmoja mwenye uwezo kama wa Chama ambaye leo angekuwa anacheza pale katikati Simba na Taifa Stars?

Ukiachana na wachache kama Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, wachezaji wanaong’ara zaidi Simba ni wa kigeni. Hata kwa washambulizi, labda Bocco awe mzima lakini naye bado hajawa na uhakika wa namba.

Simba si jukumu lao kulazimisha kusajili wazawa tu, ni klabu yenye malengo yake na imejipanga kufanya jambo fulani. Hivyo mfano Ilamfya na Salamba wangefanya vema na wengine wa mfano wao, leo wangekuwa tegemeo Simba na Taifa Stars, lakini wakambwela.


Kuna wengi mfano wa Salamba na Ilamfya lakini kinachonishangaza, hivi hawaoni? Na kama wanaona hawana hata wivu wa maendeleo? Hadi lini itakuwa hivi na kwanini wale wachezaji wa zamani walifikia hadi hatua ya makundi wakiwa na wachezaji wachache sana wa kigeni. Kama iliwezekana kipindi hicho tukawa na wachezaji wengi wazawa na mafanikio yakapatikana, vipi washindwe sasa? Wachezaji wa kipindi hiki kwani wana tatizo gani?


Kuna kila sababu ya wachezaji wazawa kujifunza hili, walifanyie kazi na wajue wamelala, wamelegea na hawataki kupambana kufikia ndoto za kuwa tegemeo katika timu zote kubwa za Tanzania.

Kwingine wameweza, Afrika Kusini lakini Kaskazini mwa Afrika kama Algeria, Misri, Tunisia na Morocco, utaona timu zao zinafanya vizuri zaidi na wazawa ndio wanaotamba zaidi katika vikosi vyao, tujifunze angalau kupitia kwao. Wageni kufanya vizuri ni jambo zuri lakini wazawa kufanya vizuri zaidi ni jambo zuri zaidi ya vizuri.

 

5 COMMENTS:

  1. Mkuu makala yako umeichambua vizuri Sana kwa manufaa ya soka letu.Lakini shida ya vijana wa cku hizi hawajitumi Kama wakina Lunyamila,Nteze John,Said Mwamba kizota,Zamoyoni Mogella au wakina Fumo Felician.Mfano Ajibu alitakiwa Mazembe akazima cm,Salamba alienda south hakujituma.Wakina Ndemla Simba hawapati nafasi Bado wanang'ang'ania kukaa bench kisa sifa za kijinga wanaandikwa magazetini.Farid Mussa alienda Spain akachemsha akarudi bongo badala ya kwenda hata Asia.Ninja Marekani akachemsha anakaa bench Yanga.Mimi nafikiri waandishi mtusaidie kuwaelimisha wachezaji wetu kuepuka sifa na starehe za kijinga .Wafundwe na Mzee Manara,Msuva,Samata na Ulimwengu kwamba ukipata golden chance itumie vema, Bila hivyo wageni wataendelea ku dominate mpira wetu.Mfano mzuri Jonas Mkude alivyoringa na kupoteza nafasi kikosi Cha kwanza Simba.Sasa hivi afanye kazi ya ziada kumtoa Muzamiru na Thadeo Lwanga

    ReplyDelete
  2. Mkuu makala yako umeichambua vizuri Sana kwa manufaa ya soka letu.Lakini shida ya vijana wa cku hizi hawajitumi Kama wakina Lunyamila,Nteze John,Said Mwamba kizota,Zamoyoni Mogella au wakina Fumo Felician.Mfano Ajibu alitakiwa Mazembe akazima cm,Salamba alienda south hakujituma.Wakina Ndemla Simba hawapati nafasi Bado wanang'ang'ania kukaa bench kisa sifa za kijinga wanaandikwa magazetini.Farid Mussa alienda Spain akachemsha akarudi bongo badala ya kwenda hata Asia.Ninja Marekani akachemsha anakaa bench Yanga.Mimi nafikiri waandishi mtusaidie kuwaelimisha wachezaji wetu kuepuka sifa na starehe za kijinga .Wafundwe na Mzee Manara,Msuva,Samata na Ulimwengu kwamba ukipata golden chance itumie vema, Bila hivyo wageni wataendelea ku dominate mpira wetu.Mfano mzuri Jonas Mkude alivyoringa na kupoteza nafasi kikosi Cha kwanza Simba.Sasa hivi afanye kazi ya ziada kumtoa Muzamiru na Thadeo Lwanga

    ReplyDelete
  3. Watz wengi kwa sasa ni wapigaji tu na hata mfumo wa malipo hauendani na viwango hivyo kuna haja kubwa ya kuangslia mifumo ya malipo kwa tija ya kumfanya mchezaji ajitume badala ya kuridhika na hill liende kwa ushirikiano wa team zote,kama fungu la nyanya mia 5 basi iwe hivyo

    ReplyDelete
  4. Tatizo kuu ni kwamba wachezaji wetu wengi hawapendi kwenda kupata changamoto nje ya nchi.Wakishacheza Simba au yanga wanaona wapo Barcelona au real Madrid.Mfano manula anatakiwa El merrikh kwa mshahara mnono lakini kutokana na mind set za wachezaji wetu hatakwenda huko Wala Mamelod wanaomtaka.John Bokho alitakiwa Algeria na akafuzu lakini hakwenda now ameanza kusota bench Simba.Tatizo ni ulimbukeni wa sifa za uongo wanazopewa magazetini na starehe za kibongo wanasahau kwamba mpira ndiyo career yao.Mindset za wachezaji wetu inabidi ziamke Kama Nigeria,Cameroon,Ghana,Uganda,Kenya au hata Congo.watoke nje ya nchi wapate changamoto ili baadaye tuwe na strong national football team.Bila hivyo west Africa,North,South na Central Africa wataendelea kutawala soccer la Africa.Wachezaji wa Kibongo amkeni! Na nyinyi waandishi endeleeni kuwaelimisha na siyo kuwapamba kwa sifa za uongo magazetini

    ReplyDelete
  5. Hatuwezi kuwa na wakina Chama bongo Kama wachezaji wetu hawatajituma.Mfano wakina Ibrahim Ajibu,Ndemla ,Kennedy Jumanne,Miraji Athuman,Dilunga wakipewa nafasi Simba wanacheza utumbo.Wanashindwa kupata wivu kutokana kwa akina Wawa,Onyango,Kagere,Mugalu,Luis,Bwalya ili coach awape nafasi zaidi ya kucheza.Mimi natabiri Manula hataondoka Simba kwa sifa anazopambwa magazetini.Nafikiri saa nyingine na Elimu inachangia maaana players wengi wa West Africa wamepiga Sana kitabu ndiyo maana kila nchi utawkuta na uchu wa maisha.Wachezaji wa Kibongo starehe nyingi mno.Manula ondoka Simba nenda El merrikh au Mamelod ukapate changamoto.Hata wakina Fei Toto,Mwamnyeto,Tshabalala ni muda wa kutoka now.Acheni mindset za wachezaji wa Zamani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic