KOCHA msaidizi wa Tanzania Prisons, Shabani Kazumba amesema wataifunga Yanga na kwenda kuchukua ubingwa wa Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ ili wawakilishe nchi kimataifa.
Kazumba maarufu kwa jina la ‘Mourinho’ amesema,” Azma yetu ni kupata uwakilishi wa kimataifa, vijana hawawezi kupata uwakilishi kama hatutacheza fainali na hatuwezi kucheza fainali kama hatuanzi kwa kuwatoa Yanga waliopo mbele yetu.
”Vijana wanakiu kubwa ya kupanda ndege, Tanzania Prisons yetu ina historia ya kuwakilisha nchi kimataifa mara kadhaa tangu nikiwa mchezaji na sasa ni kocha nahitaji kuona naiwezesha timu hii kucheza kimataifa” aliongeza Mourinho.
Tanzania Prisons watakabiliana na Yanga katika hatua ya 16 bora ya michuano ya Shirikisho yanayodhaminiwa na Azam ambayo hutoa wawakilishi wa kimataifa kwa upande wa kombe la shirikisho la soka barani Africa CAF.
Takwimu zinaonesha Tanzania Prisons imewakilisha michuano ya kimataifa mara tatu, ikiwemo mwaka 2000 baada ya kutwaa ubingwa wa Muungano na walipangiwa Ferrovirio ya Msumbiji wakatolewa na mwaka 2004 wakawakilisha kimataifa kwa kucheza na timu ya Madagascar, mara ya mwisho kwao ilikuwa 2009 walipowakilisha nchi na kutolewa mapema na timu toka Libya.
Mpira wenu ni kuzifunga yanga, simba, mkitoka kwenu mnapigwa kama mmesimama
ReplyDeleteNyie mchapeni tu ila kombe msahau
ReplyDelete