KUELEKEA kwenye mchezo wa kesho Mei Mosi, ambao ni wa Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora, Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku dhidi ya Kagera Sugar, uongozi wa Simba umewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi.
Haji Manara, Ofisa Habari wa Simba amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi huku akionesha masikitiko yake kwa mashabiki wa Dar kutojitokeza kwa wingi. Pia ameahidi kuwa ikiwa watajitokeza kwa wingi mchezo wao wa Mei 8( Simba v Yanga) watashinda zaidi ya mabao matatu.
0 COMMENTS:
Post a Comment