UWANJA wa Nelson Mandela umeshuhudia kikosi cha Yanga kikisepa na ushindi kwa mara ya kwanza mbele ya Tanzania Prisons.
Mchezo wa leo ulikuwa ni wa Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora ambapo baada ya dakika 90, ubao ulisoma Prisons 0-1 Yanga.
Ni Yacouba Songne alipachika bao hilo la ushindi kipindi cha pili dakika ya 53 na kuipa kuwanyanyua mashambiki wa timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi.
Mchezo wa kwanza ambao ulikuwa wa ligi walipokutana Uwanja wa Nelson Mandela timu zote ziligawana pointi mojamoja kwa kufunngana bao 1-1 zama za Cedric Kaze.
Baada ya mchezo huo, kiungo mshambuliaji wa Yanga, Saido Ntibanzokiza amesema kuwa kwao ni furaha kusonga mbele na ni ushindi wa timu nzima kiujumla.
"Tumepata ushindi ninafurahi naamini hii ni furaha ya wachezaji kiujumla pamoja na benchi la ufundi," amesema.
Hongereni sana..tunaelekea kuzuri
ReplyDeleteInasemekana imepenya kimipango
ReplyDeleteMilioni 40 imetembea.Refa kasema HAONI.
ReplyDeleteUna uhakika na usemalo?
Deletekujisaidia ajisaidie bata tu akijisaidia kuku amehrisha mtani acha majungu banaaaa
ReplyDelete