LEO Aprili 13, Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea ikiwa ni mzunguko wa pili na jumla ya wanaume 22 wataingia uwanjani kusaka pointi tatu muhimu.
Ni Biashara United iliyo nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa na pointi zake 20 itamenyana na Coastal Union iliyo 13 na pointi zake ni 27.
Zote zimecheza jumla ya mechi 24 kwenye ligi huku vinara wakiwa ni Yanga na pointi zao ni 51.
Biashara United imetoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Polisi Tanzania na inakutana na Coastal Union iliyotoka kupoteza kwa kufungwa mabao 4-0 dhidi ya Gwambina FC.
Mchezo wa leo utachezwa Uwanja wa Karume, Mara majira ya saa 10:00.
Biashara point 20 nafasi ya 4, Coastal point 27 nafasi ya 13... Tutaelewana tu
ReplyDeleteJaa ni mwongo sana saleh jembe
Delete